Ujumuishaji kwa Watengenezaji ============================= Ujumuishaji wa Zcash unategemea aina ya bidhaa unayojenga. Huduma inayohitaji malipo ya wazi tu inaweza kufanana na Bitcoin integration. Huduma inayotaka faragha ya Zcash inahitaji kutumia API zinazounga mkono anwani zilizolindwa. Njia mbili kuu -------------- Bitcoin-compatible approach Inafaa kama tayari una miundombinu ya Bitcoin Core na unahitaji anwani za wazi pekee. Njia hii ni rahisi kuanza nayo, lakini haitoi faida kuu ya faragha ya Zcash. Zcash API approach Inafaa kwa bidhaa mpya au huduma zinazohitaji kutuma na kupokea kupitia anwani za wazi na zilizolindwa. Hii ndiyo njia bora kama faragha ni sehemu ya bidhaa. Mtiririko wa development ------------------------- #. Anza na regtest ya ndani ili tests zisitegemee faucet. #. Thibitisha mtiririko wa anwani, kutuma, mining, na balance. #. Ongeza testnet pale tu unapohitaji kuwasiliana na mtandao wa umma. #. Kabla ya mainnet, hakiki backup, key handling, logging, na monitoring. Mfano wa RPC ------------ Mfano wa ``z_sendmany`` kwa ``curl``:: curl --user "$USER:$PASSWORD" \ -X POST \ --data-binary "{ \"jsonrpc\": \"1.0\", \"id\":\"curltest\", \"method\": \"z_sendmany\", \"params\": [\"$FROM_ADDR\", [{\"address\": \"$TO_ADDR\", \"amount\": $AMOUNT}]] }" \ -H "Content-Type: text/plain;" \ http://127.0.0.1:8232 Kwa development ya ndani kwenye repo hii, tumia port ``18232`` na credentials za mfano wa regtest. Mambo ya kuangalia ------------------ * Usilog private keys, seed phrases, au full wallet backups. * Tofautisha mainnet, testnet, na regtest kwenye config na UI. * Hakikisha ada na confirmations zinashughulikiwa wazi. * Kwa anwani zilizolindwa, panga jinsi ya kushughulikia memos na viewing keys. * Andika tests zinazoweza kurudiwa bila kutegemea faucet ya umma.